Jumanne 23 Juni 2026 - 00:00
Kauli ya ajabu kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Bahrain

Hawza/ Wakati serikali ya Bahrain ikiendelea kwa nguvu kubwa na ukandamizaji wa kikatili dhidi ya Mashia wa nchi hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Bahrain, amedai kuwa nchi hiyo inaheshimu utofauti wa kidini.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Abdul Latif Al-Zayani, Waziri wa Mambo ya Nje wa Bahrain, katika kauli zinazokinzana, alidai kuwa Bahrain inaendelea kuimarisha nafasi yake kama mfano wa kimataifa wa uvumilivu na kuishi pamoja kwa amani, kwa kuimarisha maelewano na kuheshimu utofauti wa kidini na kitamaduni.

Hali hii inajitokeza wakati ambao, sambamba na madai hayo, kampeni za kukamatwa kiholela wanazuoni na raia wa Kishia zinaendelea kuongezeka, pamoja na kufukuzwa kwa lazima, kunyang’anywa uraia, na pia kulengwa wahubiri wa mimbar za kidini.

Vilevile, serikali ya Bahrain imeendelea kwa njia ya kimfumo kutekeleza ubaguzi na ukandamizaji wa kimadhehebu, huku ikidumisha mazingira ya ukandamizaji, kunyimwa haki na kutengwa kisiasa dhidi ya Mashia.

Zaidi ya hayo, serikali hiyo imekataa kujenga upya zaidi ya misikiti 38 ya Mashia nchini humo ambayo ilibomolewa na vikosi vya kijeshi kwa msaada wa majeshi ya Saudi Arabia; vikosi ambavyo vilishiriki katika kukandamiza maandamano ya Mapinduzi ya tarehe 14 Februari 2011.

Aidha, Swala ya Ijumaa ya pamoja katika Msikiti wa Imam Sadiq (as) uliopo katika eneo la Diraz imepigwa marufuku kwa zaidi ya wiki themanini mfululizo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha